• HABARI MPYA

  Wednesday, March 06, 2024

  SIMBA SC CHALI JAMHURI, YAPIGWA 2-1 NA PRISONS


  WAKITUMIA Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro kama wa nyumbani kwa mara nyingine leo, Simba SC imechapwa mabao 2-1 na Tanzania Prisons katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania.
  Mabao yote ya Tanzania Prisons yamefungwa na mshambuliaji Samson Baraka Mbangula dakika ya 45 na ushei na 62, huku bao pekee la Simba likifungwa na kiungo Mkongo, Fabrice Luamba Ngoma dakika ya 89.
  Kwa ushindi huo, Tanzania Prisons wanafikisha pointi 27 katika mchezo wa 19 na kusogea nafasi ya nne, wakati Simba SC inabaki na pointi zake 36 za mechi 16 sasa nafasi ya tatu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA SC CHALI JAMHURI, YAPIGWA 2-1 NA PRISONS Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top