• HABARI MPYA

  Wednesday, March 20, 2024

  CHANGALAWE NAYE ATINGA NUSU FAINALI NDONDI ALL AFRICAN GAMES


  BONDIA wa Tanzania, Yussuf Changalawe amefanikiwa kutinga Nusu Fainali katika Mchezo ya Afrika (All African Game) inayoendelea nchini Ghana baada ya kumshinda Maxinillano Bibano wa Equatorial Guinea uzito wa 
  Light Heavy kufuatia Refa Kusimamisha Pambano (RSC) Raundi ya kwanza tu kumnusuru na kipigo zaidi mpinzani ukumbi wa Bukom Arena Jijini Accra. 
  Kwa ushindi huo, Changalawe ambaye ni Nahodha wa timu hiyo ya taifa ya ndondi inayojulikana kama Faru Weusi wa Ngorongoro  amejihakikishia kushinda Medali kwenye michezo ya Mwaka huu nchini Ghana na sasa atakutana na Pita Kabeji wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) katika Nusu Fainali.
  Mabondia wengine wa Tanzania waliotinga Nusu Fainali na kujihakikishia Medali ni Ezra Paul Mwanjwango uzito wa Light na  waliofanya hivyo ni Musa Maregesi uzito wa Cruiser.
  Na hii ni maana yake Ahadi ya Rais wa Shirikisho la Ngumi Tanzania (BFT), Anderson Lukelo Willilo kurejea nchini na Medali nyingi inaelekea kabisa kutimia.
  “Vijana walijiandaa vizuri, kazi iliyokuwa imebakia tulimkabidhi Mungu tu, Mweza wa yote, hakika tunamshukuru kwa hatua tuliyofikia mpaka sasa pamoja na Dua za Watanzania wote waliotuombea mema,” alisema Willilo.

  Yusuf Changalawe (wa pili kulia) amejihakikishia Medali All African Games. Wengine pichani kutoka kushoto ni viongozi wa Shirikisho la Ngumi za Ridhaa Tanzania (BFT), Katibu Mkuu Makore Mashaga na Raisi, Lukelo Willilo. Kulia Kocha Mkuu wa timu ya taifa ya Ndondi za Ridhaa Tanzania, Samwel Kapungu ‘Batman’ na hii ilikuwa ni  Jijini Dakar nchini Senegal Septemba mwaka jana kwenye Mashindano ya kufuzu Olimpiki kwa Bara la Afrika.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: CHANGALAWE NAYE ATINGA NUSU FAINALI NDONDI ALL AFRICAN GAMES Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top