• HABARI MPYA

  Sunday, October 02, 2022

  MTIBWA SUGAR NA MBEYA CITY SARE 2-2 MANUNGU


  WENYEJI, Mtibwa Sugar wamelazimishwa sare ya 2-2 na Mbeya City katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara leo Uwanja wa Manungu, Turiani mkoani Morogoro.
  Mabao ya Mtibwa Sugar yamefungwa na Nickson Kibabage dakika ya kwanza na Jean Papi Matore dakika ya 29, wakati ya Mbeya City kipa Farouk Shikaro alijifunga dakika ya 55 na Tariq Seif akafunga la pili was dakika ya 65.
  Kwa matokeo hayo, Mtibwa Sugar inafikisha pointi nane, ingawa inabaki nafasi ya saba na Mbeya City inafikisha pointi tano katik nafasi ya 11 baada ya wote kucheza mechi tano.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MTIBWA SUGAR NA MBEYA CITY SARE 2-2 MANUNGU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top