• HABARI MPYA

  Sunday, October 02, 2022

  SIMBA SC YAIPIGA DODOMA JIJI 3-0 NA KUPANDA KILELENI

  VIGOGO, Simba SC wamepanda kileleni mwa Ligi Kuu ya Tanzania Bara kufuatia ushindi wa 3-0 dhidi ya Dodoma Jiji FC leo Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam. 
  Beki wa Yanga anayecheza kwa mkopo Dodoma Jiji, Abdallah Shaibu 'Ninja' alijifunga dakika ya tano tu kuipatia Simba bao la kwanza, kabla ya washambuliaji, Mzambia Moses Phiri kufunga la pili dakika ya 45 na mzawa, Habib Kyombo la tatu dakika ya 85.
  Kwa ushindi huo, Simba SC wanafikisha pointi 13 na kupanda juu ya msimamo wa Ligi, wakiizidi pointi mbili Namungo FC inayofuatia baada ya wote kucheza mechi tano, wakati mabingwa watetezi wanashukia nafasi ya tatu kwa pointi zao 10 za mechi nne.
  Kwa upande wao Dodoma Jiji ambao leo wamecheza mechi ya sita, wanabaki na pointi zao tano katika nafasi ya 11. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA SC YAIPIGA DODOMA JIJI 3-0 NA KUPANDA KILELENI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top