• HABARI MPYA

  Sunday, October 02, 2022

  HAALAND APIGA HAT TRICK TENA MAN CITY YAIFUMUA UNITED 6-3


  WENYEJI, Manchester City wameitandika Manchester United mabao 6-3 katika mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa Etihad Jijini Manchester.
  Mabao ya Man City yamefungwa na Phil Foden matatu dakika ya nane, 44 na 72 na Erling Haaland matatu pia dakika za 34, 37 na 64, wakati ya Man United yamefungwa na Antony dakika ya 56 na Anthony Martial  mawili dakika ya 84 na 90 na ushei kwa penalti.
  Kwa ushindi huo, Man City wanafikisha pointi 20, ingawa wanabaki nafasi ya pili wakizidiwa pointi moja na Arsenal, wakati Man United inabaki na pointi zake 12 nafasi ya sita baada ya wote kucheza mechi saba.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: HAALAND APIGA HAT TRICK TENA MAN CITY YAIFUMUA UNITED 6-3 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top