• HABARI MPYA

  Friday, September 08, 2023

  TAIFA STARS OYEEE, YAFUZU AFCON MWAKANI IVORY COAST


  TIMU ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars imekata tiketi ya kucheza Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) mwakani, 2024 baada ya sare ya bila kufungana na wenyeji, Algeria katika mchezo wa mwisho wa Kundi F usiku huu Uwanja wa Mei 19, 1956 mjini Annaba.
  Kwa matokeo hayo Taifa Stars inamaliza na pointi nane, nyuma ya vinara, Algeria wenye pointi 16 na wote wanafuzu AFCON ya Ivory Coast 2024 wakizipiku Uganda iliyomaliza na pointi saba na Níger pointi mbili.
  Mechi nyingine ya mwisho ya Kundi F leo Níger wamechapwa mabao 2-0 na Uganda Uwanja wa Marrakech nchini Morocco.
  Hii inakuwa mara ya tatu kihistoria kwa Tanzania kufuzu AFCON baada ya mwaka 1980 nchini Nigeria na 2019 nchini Misri.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: TAIFA STARS OYEEE, YAFUZU AFCON MWAKANI IVORY COAST Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top