• HABARI MPYA

  Friday, September 22, 2023

  WAZIRI NDUMBARO AIAGIZA MIKOA KUJIANDAA VYEMA MASHINDANO YA SAMIA TAIFA CUP


  WAZIRI wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk. Damas Ndumbaro ameiagiza Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kujiandaa vyema kwa ajili ya mashindano ya Samia Taifa Cup ambayo yatafanyika mwishoni mwa mwaka huu.
  Ndumbaro ametoa maagizo hayo Septemba 21, 2023 Zanzibar wakati akikabidhi  vifaa vya michezo kwa wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kwa ajili ya maandalizi ya  mashindano hayo ambayo yatahusisha michezo mbalimbali.
  "Mwaka huu mashindano yatajumuisha pia Zanzibar na kutakua na Mashindano ya Muziki wa Kizazi Kipya. Lengo la mashindano haya ni kuendelea kuenzi Muungano wetu na  kuhakikisha jamii inajishughulisha na michezo, Sanaa  na Utamaduni kwakua ni Sekta ambazo zinaibua vipaji na kutoa fursa ya ajira" amesema Mhe. Ndumbaro.
  Kwa upande wake Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Tabia Maulid Mwita amesema  vifaa hivyo vitagawiwa katika mikoa yote ya Zanzibar na mashindano yataanzia katika ngazi ya Shehia mpaka Mkoa ili kupata wawakilishi wazuri Kitaifa.
  Miongoni mwa vifaa alivyokabidhi Mhe. Ndumbaro ni pamoja na mipira ya  michezo ya mpira wa Miguu, Kikapu na Wavu ambayo kila mchezo mipira 18 huku akiwakaribisha wadau kuiunga mkono jambo hilo katika michezo mingine.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: WAZIRI NDUMBARO AIAGIZA MIKOA KUJIANDAA VYEMA MASHINDANO YA SAMIA TAIFA CUP Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top