• HABARI MPYA

  Wednesday, September 20, 2023

  MANCHESTER CITY YAWAKANDA RED STAR BELGRADE 3-1 ETIHAD


  WENYEJI, Manchester City wameibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Red Star Belgrade ya Serbia katika mchezo wa Kundi G usiku wa jana Uwanja wa Etihad Jijini Manchester.
  Ni wageni, Red Star waliotangulia na bao la kiungo Mghana, Osman Bukari dakika ya 45, kabla ya mabingwa watetezi kuzinduka na mabao ya Julian Alvarez mawili dakika ya 47 na 60 na Rodri dakika ya 73.
  Mechi nyingine ya Kundi hilo, RB Leipzig ya Ujerumani iliwachapa wenyeji, Young Boys mabao 3-0 Uwanja wa Wankdorf mjini Bern, Uswisi.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MANCHESTER CITY YAWAKANDA RED STAR BELGRADE 3-1 ETIHAD Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top