• HABARI MPYA

  Saturday, September 30, 2023

  GREEN WARRIORS, POLISI TANZANIA NA STAND UNITED ZATAMBA CHAMPIONSHIP


  TIMU ya Stand United imeibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya Copco United ya Mwanza katika mchezo wa  Ligi ya NBC Championship leo Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga.
  Mechi nyingine za Ligi ya NBC Championship Green Warriors imeichapa FGA Talents 2-0 Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam na Polisi Tanzania wameichapa Transit Camp 2-1 Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.
  Ikumbukwe jana Pamba FC ya Mwanza ililazimisha sare ya kufungana bao 1-1 na wenyeji, Biashara United Uwanja wa Karume mjini Musoma mkoani Mara, huku TMA ikiwachapa wenyeji, Pan Africans 2-1 Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: GREEN WARRIORS, POLISI TANZANIA NA STAND UNITED ZATAMBA CHAMPIONSHIP Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top