• HABARI MPYA

  Tuesday, September 05, 2023

  HUKO BUNJU SIMBA IMEMPIGA MTU MKONO ASUBUHI YA LEO


  TIMU ya Simba SC imeibuka na ushindi wa mabao 5-1 dhidi ya Cosmopolitan FC katika mchezo wa kirafiki asubuhi ya leo Uwanja wa Mo Simba Arena, Bunju Jijini Dar es Salaam.
  Mabao ya Simba SC katika mchezo dhidi ya timu ya Championship yamefungwa na nyota wake, Mzambia Moses Phiri, Mkongo Jean Baleke, Mcameroon Leandre Willy Essomba Onana, Muivory Coast, Aubin Kramo Kouamé na mzawa Shaaban Iddi Chilunda.
  Simba SC inajiandaa na mchezo kwanza Hatua ya mwisho ya kufuzu Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Power Dynamos Septemba 15 Jijini Ndola nchini Zambia. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: HUKO BUNJU SIMBA IMEMPIGA MTU MKONO ASUBUHI YA LEO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top