• HABARI MPYA

  Friday, September 15, 2023

  DODOMA JIJI YAAMBULIA SARE 1-1 NA MTIBWA SUGAR


  WENYEJI, Dodoma Jiji FC wamelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na majirani, Mtibwa Sugar ya Morogoro katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.
  Ni wageni waliotangulia kwa bao la dakika ya 18 la Abdul Hillary kabla ya Emmanuel Martin kuisawazishia Dodoma Jiji FC dakika ya 38.
  Kwa matokeo hayo, Dodoma Jiji inafikisha pointi nne, wakati Mtibwa Sugar wanatimiza pointi mbili tu baada ya wote kucheza mechi tatu.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: DODOMA JIJI YAAMBULIA SARE 1-1 NA MTIBWA SUGAR Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top