• HABARI MPYA

  Friday, September 22, 2023

  STAND UNITED WAICHAPA PAMBA 1-0, PAN AFRICAN YAPIGWA UHURU


  WENYEJI, Stand United wameibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya Pamba FC ya Mwanza, bao pekee la Emmanuel Mtambuka dakika ya 55 katika mchezo wa Ligi ya NBC Championship leo Uwanja wa CCM Kambarage mjini Shinyanga.
  Mechi nyingine ya NBC Championship leo Mbuni FC ya Arusha imewazima wenyeji, Pan African kwa kuwachapa 1-0 Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.
  Mbuni FC wanapanda kileleni wakifikisha pointi saba, Pamba FC inashukia nafasi ya tatu ikibaki na pointi sita, Stand United pointi nne nafasi ya nane na Pan Africans nafasi ya 11 pointi tatu baada ya wote kucheza mechi tatu.   
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: STAND UNITED WAICHAPA PAMBA 1-0, PAN AFRICAN YAPIGWA UHURU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top