• HABARI MPYA

  Tuesday, September 26, 2023

  SIMBA SC YAWATANDIKA PAN AFRICANS 4-0 BUNJU


  TIMU ya Simba SC imeibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Pan Africans katika mchezo wa kirafiki leo Uwanja wa Mo Simba Arena, Bunju Jijini Dar es Salaam.
  Mabao ya Simba SC leo yamefungwa na Mrundi Saido Ntibanzokiza, Mzambia Moses Phiri, Kibu Dennis na Mcameroon Andre Onana.
  Simba imeutumia mchezo huo kama sehemu ya maandalizi yao ya mchezo wao wa marudiano hatua ya 32 Bora Ligi ya Mabingwa Afrika Jumapili dhidi ya Power Dynamos ya Zambia Jumapili.
  Simba inahitaji angalau ushindi wa 1-0 au sare isiyozidi 1-1 na Power Dynamos ili kwenda hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya sare ya 2-2 kwenye mechi ya kwanza Jumamosi iliyopita.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA SC YAWATANDIKA PAN AFRICANS 4-0 BUNJU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top