• HABARI MPYA

  Saturday, September 16, 2023

  CHAMA ASAWAZISHA MARA MBILI SIMBA YATOA DROO 2-2 ZAMBIA


  TIMU ya Simba SC imetoa sare ya kufungana mabao 2-2 na wenyeji, Power Dynamos katika mchezo wa kwanza wa Hatua ya 32 Bora Ligi ya Mabingwa Afrika leo Uwanja wa Levy Mwanawaswa Jijini Ndola nchini Zambia.
  Mabao ya Power Dynamos la kwanza beki Mkongo Henock Inonga Baka aliubadili mweleko mpira uliopigwa na Joshua Mutale katika harakati za kuokoa dakika ya 28 ukampita kipa Mmorocco, Ayoub Lekred na la pili likafungwa na Cephas Mulombwa dakika ya 74, wakati mabao yote ya Simba yamefungwa na kiungo Mzambia Clatous Chotta Chama dakika ya 62 na 90.
  Timu hizo zitarudiana Jijini Dar es Salaam Jumapili ijayo na mshindi wa jumla atakwenda hatua ya 16 Bora ambayo itachezwa kwa mfumo wa makundi.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: CHAMA ASAWAZISHA MARA MBILI SIMBA YATOA DROO 2-2 ZAMBIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top