• HABARI MPYA

  Saturday, September 09, 2023

  JKU WAICHAPA KMKM 5-2 KUTWAA NGAO YA JAMII ZANZIBAR


  TIMU ya JKU imefanikiwa kutwaa Ngao ya Jamii Zanzibar baada ya ushindi wa mabao 5-2 dhidi ya mabingwa wa Ligi Kuu ya PBZ visiwani humo, KMKM leo Uwanja wa Mao Dze Tung, Unguja.
  Mabao ya JKU, washindi wa Kombe la FA Zanzibar yamefungwa na Saleh Masoud dakika ya tano, Nassor Mattar dakika ya 22, Gamba Iddi dakika ya 32 na Saleh Karabaka dakika ya 75 na 90, wakati ya KMKM yamefungwa na Salum Mussa dakika ya kwanza na Isihaka Ibrahim dakika ya 73.
   
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: JKU WAICHAPA KMKM 5-2 KUTWAA NGAO YA JAMII ZANZIBAR Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top