• HABARI MPYA

  Friday, September 29, 2023

  COASTAL UNION NA TABORA UNITED HAKUNA MBABE, 0-0 MKWAKWANI


  TIMU ya Coastal Unión imelazimishwa sare ya bila mabao na Tabora United katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Mkwakwani Jijini Tanga.
  Tabora United, zamani Kitayosce inafikisha pointi tano na kusogea nafasi ya tano, wakati Coastal Unión inafikisha pointi mbili na kusogea nafasi ya 14 baada ya wote kucheza mechi nne.
  Mechi nyingine ya Ligi Kuu leo, JKT Tanzania imelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Kagera Sugar Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga.
  Mshambuliaji Daniel Lyanga alianza kuifungia JKT Tanzania kwa penalti dakika ya sita ya muda wa ziada baada ya kutimia dakika 90, kabla ya Gasper Mwaipasi kuisawazishia Kagera Sugar dakika mbili baadaye.
  Timu zote zinafikisha pointi katika michezo minne, Kagera Sugar nafasi ya nane na JKT Tanzania nafasi ya 10.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: COASTAL UNION NA TABORA UNITED HAKUNA MBABE, 0-0 MKWAKWANI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top