• HABARI MPYA

  Saturday, September 30, 2023

  WOLVES WAWAKANDA MABINGWA WATETEZI MAN CITY 1-0 MOLINEUX


  MABINGWA watetezi, Manchester City wamepoteza mchezo wa kwanza wa msimu wa Ligi Kuu ya England baada ya kuchapwa mabao 2-1 na wenyeji, Wolverhampton Wanderers leo Uwanja wa Molineux mjini Wolverhampton, West Midlands.
  Mabao ya Wolverhampton Wanderers leo yamefungwa na Rúben Dias aliyejifunga dakika ya 13 na Hwang Hee-Chan dakika ya 66, wakati bao pekee la Manchester City limefungwa na Julián Álvarez dakika ya 58.
  Wolverhampton Wanderers wanafikisha pointi saba na kusogea nafasi ya 13, wakati Manchester City wanabaki na pointi zao 18 na kuendelea kuongoza Ligi kwa pointi moja zaidi ya Arsenal baada ya wote kucheza mechi saba.
  Liverpool ina nafasi ya kupanda kileleni baadaye kama itawafunga wenyeji Tottenham Hotspur.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: WOLVES WAWAKANDA MABINGWA WATETEZI MAN CITY 1-0 MOLINEUX Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top