• HABARI MPYA

  Monday, September 25, 2023

  SERENGETI GIRLS YAICHAPA TENA MOROCCO 2-1 CHAMAZI


  TIMU ya taifa ya wasichana chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Girls imeibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Morocco U17 katika mchezo wa kirafiki leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam.
  Mabao yote ya Serengeti Girls yamefungwa na Jamila Rajab baada ya Morocco kutangulia kwa bao la Elanbri Alisha.
  Huo ulikuwa mchezo wa marudiano baada ya mchezo wa kwanza Serengeti Girls kushinda pia 2-1 mabao yake yakifungwa na Masika Khing na Sabina Alex, huku la Morocco U17 likifungwa na Bentahri Ovafaa.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SERENGETI GIRLS YAICHAPA TENA MOROCCO 2-1 CHAMAZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top