• HABARI MPYA

  Wednesday, September 13, 2023

  CHANGALAWE AMTWANGA MSENEGAL NA KUTINGA NUSU FAINALI KUFUZU OLIMPIKI


  BONDIA Yusuf Changalawe amefanikiwa kutinga Nusu fainali ya Mashindano ya kuwania tiketi ya kucheza Michezo ya Olimpiki mwakani Paris baada ya kumshinda kwa points 4-1 mwenyeji, Seydina Konate leo Jijini Dakar nchini Senegal. 
  Lilikuwa pambano la uzito wa Light Heavy na sasa Nahodha huyo wa Tanzania, Changalawe ametinga hatua ya nusu fainali ambayo atacheza kesho.
  Mabondia wengine wa Tanzania waliocheza awali ya leo katika hatua ya robo fainali walipoteza ambapo Abdallah Katoto dhidi ya Said Mortaji kutoka Morocco kwa points 4-1 katika bout no 166 uzani wa 51kg na Grace Mwakamele kwa RSC round ya kwanza dhidi ya Imane Khelif kutoka Algeria katika bout no. 165 uzani wa 66kg.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: CHANGALAWE AMTWANGA MSENEGAL NA KUTINGA NUSU FAINALI KUFUZU OLIMPIKI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top