• HABARI MPYA

  Saturday, September 09, 2023

  SIMBA SC YAITANDIKA NGOME 6-0 BALEKE AFUNGA MAWILI


  KLABU ya Simba leo imeibuka na ushindi wa mabao 6-0 dhidi ya timu ya Ngome katika mchezo wa kirafiki Uwanja wa Mo Simba Arena, Bunju Jijini Dar es Salaam.
  Mabao ya Simba yamefungwa na beki Shomari Kapombe, kiungo Muivory Coast, Aubin Kramo Kouame, washambuliaji Mkongo Jean Othos Baleke mawili, Mcameroon Leandre Willy Essomba Onana na mzawa, Shaaban Iddi Chilunda.
  Simba SC inajiandaa namchezo wao wa kwanza hatua ya mwisho ya mchujo wa kuwania kucheza 16 Bora ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya wenyeji, Power Dynamos Septemba 16 Uwanja wa Levy Mwanawasa Jijini Ndola.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA SC YAITANDIKA NGOME 6-0 BALEKE AFUNGA MAWILI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top