• HABARI MPYA

  Thursday, September 21, 2023

  MAN UNITED YACHAPWA 4-3 NA BAYERN MUNICH UJERUMANI


  TIMU ya Manchester United imeanza vibaya michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kuchapwa mabao 4-3 na wenyeji, Bayern Munich katika mchezo wa Kundi A usiku wa Jana Uwanja wa Allianz Arena Jijini Múnich nchini Ujerumani.
  Mabao ya Bayern Munich yamefungwa na Leroy Sané dakika ya 28, Serge Gnabry dakika ya 32, Harry Kane kwa penalti dakika ya 53 na Mathys Henri Tel dakika ya 90 na ushei.
  Kwa upande wao, Manchester United mabao yao yamefungwa na Rasmus Højlund dakika ya 49 na Carlos Henrique Casemiro dakika ya 88 na 90.
  Mchezo mwingine wa Kundi A, wenyeji Galatasaray walitoka sare ya 2-2 na FC Copenhagen Uwanja wa Rams Global mjini İstanbul nchini Uturuki.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAN UNITED YACHAPWA 4-3 NA BAYERN MUNICH UJERUMANI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top