• HABARI MPYA

  Saturday, September 30, 2023

  ARSENAL YAIKUNG’UTA BOURNEMOUTH 4-0 VITALITY


  TIMU ya Arsenal imeibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya wenyeji, AFC Bournemouth katika mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa Vitality mjini Bournemouth, Dorset.
  Mabao ya Arsenal yamefungwa na Bukayo Saka dakika ya 17, Martin Ødegaard kwa penalti 44, Kali Havertz kwa penalti pia dakika ya 53 na Benjamin White dakika ya 90 na ushei.
  Kwa ushindi huo, Arsenal inafikisha pointi 17 na kusogea nafasi ya pili, ikizidiwa pointi moja na mabingwa watetezi, Manchester City, wakati AFC Bournemouth inabaki na pointi zake tatu nafasi ya 18 baada ya wote kucheza mechi saba.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ARSENAL YAIKUNG’UTA BOURNEMOUTH 4-0 VITALITY Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top