• HABARI MPYA

  Saturday, September 16, 2023

  LIVERPOOL YATOKA NYUMA KUICHAPA WOLVES 3-1


  TIMU ya Liverpool imetoka nyuma na kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya wenyeji, Wolverhampton Wanderers katika mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa Molineux, West Midlands.
  Wolves walitangulia na bao la Hwang Hee-Chan dakika ya saba, kabla ya Liverpool kuzinduka kwa mabao ya Cody Gakpo dakika ya 55, Andy Robertson dakika ya 85 na Hugo Bueno aliyejifunga dakika ya 90 na ushei. 
  Kwa ushindi huo, Liverpool inafikisha pointi 13 ikienda nafasi ya tatu, wakati Wolves inabaki na pointi zake tatu nafasi ya 15 baada ya wote kucheza mechi tano.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: LIVERPOOL YATOKA NYUMA KUICHAPA WOLVES 3-1 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top