• HABARI MPYA

  Saturday, September 30, 2023

  AZAM FC YAPATA MSIBA, DEREVA WAKE KAWEMBA AFARIKI DUNIA


  KLABU ya Azam FC imepata msiba wa kufiwa na mfanyakazi wake, Kawemba Saad, aliyefariki dunia leo Jumamosi asubuhi, akiwa kwenye matibabu, visiwani Zanzibar.
  “Tunatuma salamu zetu za rambirambi kwenda kwa familia ya marehemu, ndugu, jamaa, marafiki na wafanyakazi wote wa Azam FC,”
  “Azam FC tutamkumbuka Kawemba, aliyekuwa dereva wa mabasi yetu, kama mmoja wa wafanyakazi wachapakazi kwa kipindi chote alichoitumikia timu yetu,”
  Msiba upo nyumbani kwa marehemu, Magomeni Makutano Mtaa wa Kagera na Kondoa na mazishi yatafanyika kesho Jumapili saa 4.00 Asubuhi, kwenye makaburi ya Mburahati.
  Inna Lillahi Wa Inna Ilayhi Rajiun! 🙏
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AZAM FC YAPATA MSIBA, DEREVA WAKE KAWEMBA AFARIKI DUNIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top