• HABARI MPYA

  Monday, September 18, 2023

  ARSENAL YAICHAPA EVERTON 1-0 PALE PALE GOODISON PARK


  TIMU ya Arsenal imeibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Everton katika mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa Goodison Park Jijini Liverpool.
  Bao pekee la Arsenal leo limefungwa na mshambuliaji wake Mbelgiji, Leandro Trossard dakika ya 69 akimalizia kazi nzuri ya Bukayo Saka na kwa ushindi huo wanafikisha pointi 13, ingawa inabaki nafasi ya nne ikizidiwa wastani wa mabao na Liverpool na Tottenham Hotspur baada ya wote kucheza mechi tano.
  Kwa upande wao Everton baada ya kipigo hicho wanabaki na pointi yao moja waliyovuna kwenye sare na Sheffield United ugenini kufuatia kufungwa mechi nyingine tatu dhidi ya Aston Villa 4-0, Wolverhampton Wanderers 1-0 na Fulham 1-0.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ARSENAL YAICHAPA EVERTON 1-0 PALE PALE GOODISON PARK Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top