• HABARI MPYA

  Sunday, September 24, 2023

  ARSENAL YANG’ANG’ANIWA NA EMIRATES, SARE 2-2 NA SPURS


  TIMU ya Arsenal imelazimishwa sare ya kufungana mabao 2-2 na Tottenham katika mechi ya mahasimu wa Kaskazini mwa London leo Uwanja wa Emirates Jijini London.
  Cristian Romero alianza kujifunga akijaribu kuokoa krosi ya Bukayo Saka dakika ya 26, kabla ya as Son Heung-min kuisawazishia Tottenham Hotspur dakika ya 42.
  Bukayo Saka akaifungia bao la pili Arsenal dakika ya 54 kwa penalti na kwa mara nyingine as Son Heung-min akaisawazishia Spurs dakika ya 55.
  Wote wanafikisha pointi 14 baada ya kucheza mechi sita, Tottenham Hotspur ikikaa nafasi ya nne na Arsenal nafasi ya tano.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ARSENAL YANG’ANG’ANIWA NA EMIRATES, SARE 2-2 NA SPURS Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top