• HABARI MPYA

  Sunday, September 24, 2023

  MBEYA KWANZA YAIFUMUA MBEYA CITY 4-0 MTWARA


  TIMU ya Mbeya Kwanza jana imepanda kileleni mwa Ligi ya NBC Championship baada ya ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Mbeya City Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara.
  Mechi nyingine za Ligi ya NBC Championship jana Cosmopolitan ililazimishwa sare ya bila kufungana na TMA Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam na Ruvu Shooting ikachapwa 3-0 na Ken Gold Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.
  Ikumbukwe juzi Stand United iliibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya Pamba FC ya Mwanza Uwanja wa CCM Kambarage mjini Shinyanga, huku Mbuni FC ya Arusha ikiwazima wenyeji, Pan African kwa kuwachapa 1-0 Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.
  Msimamo wa Ligi ya NBC Championship sasa ni Mbeya Kwanza, Ken Gold na Mbuni FC zote zipo juu kila timu ikiwa na pointi saba baada ya wote kucheza mechi tatu. 
  Ligi hiyo inaendelea leo kwa mechi nyingine tatu kukamilisha mzunguko wa tatu; Green Warriors na Polisi Tanzania Uwanja wa Uhuru, Transit Camp na FGA Talents Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro na Biashara United dhidi ya COPCO Uwanja wa Karume, Musoma mkoani Mara.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MBEYA KWANZA YAIFUMUA MBEYA CITY 4-0 MTWARA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top