• HABARI MPYA

  Wednesday, September 13, 2023

  TANZANIA KUSHIRIKIANA NA MOROCCO KATIKA MICHEZO


  WAZIRI wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Damas Ndumbaro amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Morocco hapa nchini Zakaria El Goumiri kuhusu ushirikiano baina ya Tanzania na Morocco katika Sekta ya Michezo.
  Kikao hicho kimefanyika Septemba 13, 2023 katika ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es Salam na Dk. Ndumbaro amewasilisha salamu za pole kwa nchi hiyo kufuatia Tetemeko la Ardhi lililopita katika nchi hiyo. Na kumhakikisha Balozi huyo kuwa, Tanzania itaendelea kuimarisha ushirikiano baina ya nchi hizo mbili. 
  Kwa upande wake  Balozi Zakaria El Goumiri amepokea salamu za pole kutoka Tanzania, ambapo pia  amesema nchi yake itaiunga mkono Tanzania katika ujenzi wa miondombinu ya michezo ili kuendelea kukuza vipaji vya wanamichezo ambao watakuwa ni hazina kwa mataifa hayo kwenye timu za taifa.
  Kikao  hicho kimehudhuriwa pia Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Saidi Yakubu ambaye amesema ushirikiano wa Tanzania na Morocco katika sekta ya michezo ni wa kihistoria na kila mara nchi hizo mbili zimekuwa na mechi za kirafiki katika nyakati tofauti na hivi karibuni timu moja kutoka nchi hiyo itakuja nchini kucheza na timu mojawapo.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: TANZANIA KUSHIRIKIANA NA MOROCCO KATIKA MICHEZO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top