• HABARI MPYA

  Friday, September 22, 2023

  LIVERPOOL YATOKA NYUMA KUSHINDA 3-1 UGENINI EUROPA LEAGUE


  TIMU ya Liverpool imetoka nyuma na kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya wenyeji, LASK usiku wa jana katika mchezo wa Kundi E UEFA Europa League Uwanja wa Raiffeisen Arena mjini Linz nchini Austria.
  Florian Flecker alianza kuifungia LASK dakika ya 14, kabla ya Liverpool kuzinduka na mabao ya Darwin Nunez dakika ya 56, Luis Diaz dakika ya 63 na Mohamed Salah dakika ya 88.
  Mechi nyingine ya Kundi E jana, wenyeji Union Saint-Gilloise walilazimishwa sare ya 1-1 na Toulouse ya Ufaransa Uwanja wa Lotto Park mjini Brussel, Ubelgiji.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: LIVERPOOL YATOKA NYUMA KUSHINDA 3-1 UGENINI EUROPA LEAGUE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top