• HABARI MPYA

  Friday, September 29, 2023

  JKT TANZANIA YAAMBULIA SARE KWA KAGERA SUGAR 1-1 KAMBARAGE


  TIMU ya JKT Tanzania imelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Kagera Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga.
  Mshambuliaji Daniel Lyanga alianza kuifungia JKT Tanzania kwa penalti dakika ya sita ya muda wa ziada baada ya kutimia dakika 90, kabla ya Gasper Mwaipasi kuisawazishia Kagera Sugar dakika mbili baadaye.
  Timu zote zinafikisha pointi katika michezo minne, Kagera Sugar nafasi ya nane na JKT Tanzania nafasi ya 10.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: JKT TANZANIA YAAMBULIA SARE KWA KAGERA SUGAR 1-1 KAMBARAGE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top