• HABARI MPYA

  Saturday, September 30, 2023

  YANGA SC YATINGA HATUA YA MAKUNDI LIGI YA MABINGWA AFRIKA


  MABINGWA wa Tanzania, Yanga wamefanikiwa kutinga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya ushindi wa 1-0 leo dhidi ya Al Merreikh ya Sudan Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam.
  Pongezi kwa mfungaji wa bao hilo pekee, mshambuliaji chipukizi Clement John Mzize dakika ya 66 kwa kichwa akiunganisha krosi ya beki Mkongo, Joyce Lomalisa Mutambala kutoka upande wa kushoto wa Uwanja.
  Yanga inakwenda hatua ya 16 Bora kwa ushindi wa jumla wa 3-0 kufuatia kuwachapa Al Merreikh 2-0 kwenye mchezo wa kwanza wiki mbili zilizopita mjini Kigali, Rwanda.
  Mara ya mwisho Yanga kwenda hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika ilikuwa mwaka 1998 wakipozitoa Rayon Sport ya Rwanda na Coffee ya Ethiopia katika Raundi mbili za awali.
  Na msimu huu Yanga wanafika Hatua hiyo baada ya kuzitoa ASAS ya Djibouti na Merreikh.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA SC YATINGA HATUA YA MAKUNDI LIGI YA MABINGWA AFRIKA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top