• HABARI MPYA

  Tuesday, September 26, 2023

  TWIGA STARS YAITOA IVORY COAST KWA MATUTA CHAMAZI


  TIMU ya taifa ya wanawake ya Tanzania imefanikiwa kutinga hatua ya mwisho ya mchujo wa kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Kombe la Mataifa ya mwakani nchini Morocco baada ya kuwatoa Ivory Coast kwa penalti 4-2 kufuatia sare ya jumla ya 2-2.
  Mchezo wa leo jioni Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam umemalizika kwa Twiga Stars kushinda 2-0, mabao ya Deonisia Minja na Opa Clement hivyo kufanya sare ya jumla ya 2-2 kufuatia Ivory Coast kushinda 2-0 pia kwenye mchezo wa kwanza Ijumaa mjini Yamoussoukro.
  Na kwenye mikwaju ya penalti Twiga Stars wakishinda 4-2 na sasa watakutana na mshindi wa jumla kati ya Djibouti na Togo zinazorudiana leo Saa 12:30 jioni mjini Lome baada ya Togo kushinda 7-0 kwenye mchezo wa kwanza ugenini.
  Wakati huo huo: Katibu mpya wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Gerson Msigwa amesema kwamba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan amewazadia Twiga Stars Sh. Milioni 10 kwa kuitoa Ivory Coast.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: TWIGA STARS YAITOA IVORY COAST KWA MATUTA CHAMAZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top