• HABARI MPYA

  Saturday, September 09, 2023

  BONDIA MWINGINE WA TANZANIA ANG'ARA DAKAR KUFUZU OLIMPIKI 2024


  BONDIA Abdallah Abdallah 'Katoto' ameanza vyema Mashindano ya kuwania kufuzu Michezo ya Olimpiki ya Paris 2024 kwa Bara la Afrika baada ya ushindi wa pointi 5-0 dhidi ya Patrick Gomes Fernandez wa Cape Verde leo katika pambano la uzito wa Fly Jijini Dakar nchini Senegal. 
  Sasa Katoto atacheza na Abdalah Saied Emam wa Misri katika hatua ya 16 Bora Jumatatu na huyo anakuwa bondia wa pili wa Tanzania kupita hatua ya kwanza baada ya Zulfa Macho Yusufu kumshinda Grace Nankinga wa Uganda kwa pointi 5-0 katika pambano la uzito wa Fly mapema leo.
  Kwa ushindi huo, binti huyo wa mwanasoka nyota nchini wa zamani aliyewika Simba, Yanga na Taifa Stars ameingia hatua ya 16 Bora na atapambana Adeiola Oyesiji wa Nigeria.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: BONDIA MWINGINE WA TANZANIA ANG'ARA DAKAR KUFUZU OLIMPIKI 2024 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top