• HABARI MPYA

  Tuesday, September 05, 2023

  AZAM FC KUCHEZA NA TIMU YA KINA KALOU NA ALEX SONG JUMAMOSI


  KLABU ya Azam FC itakuwa na mchezo wa kirafiki dhidi ya Arta Solar ya Djibouti Jumamosi kuanzia Saa 11:00 jioni Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam.
  Miongoni mwa nyota wa Arta Solar ni winga wa zamani wa Kimataifa wa Ivory Coast, Salomon Armand Magloire Kalou aliyewika klabu za Feyenoord, Excelsior za Uholanzi, Chelsea ya England, Hertha Berlin ya Ujerumani na Botafogo ya Brazil enzi zake.
  Lakini kikosini ina wakali wengine pia kama kiungo wa zamani wa Arsenal ya England na Barcelona ya Hispania, Mcameroon Alex Song, Muivory Coast mwingine, beki Gilles N'Guessan aliyewahi kuwika African Sports na ASEC Mimosas sa kwao na kipa Mganda, Sulait Luyima.
  Wapo pia mshambuliaji wa Kimataifa wa Burkina Faso, Alain Traoré aliyewahi kuchezea Auxere na Monaco za Ufaransa na Kipa Mfaransa Christopher Dilo aliyewahi kuchezea Blackburn Rovers ya England, Sochaux na Paris FC za kwao pamoja na timu ya taifa ya Guadeloupe.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AZAM FC KUCHEZA NA TIMU YA KINA KALOU NA ALEX SONG JUMAMOSI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top