• HABARI MPYA

  Saturday, September 16, 2023

  CHANGALAWE APOTEZA FAINALI, ASHINDA MEDALI YA FEDHA DAKAR


  BONDIA Yusuf Changalawe wa Tanzania amepoteza pambano la Fainali ya kuwania tiketi ya kucheza Michezo ya Olimpiki mwakani Jijini Paris, Ufaransa baada ya kushindwa kwa pointi na Abdelrahman Abdelgawwad wa Misri katika pambano la uzito wa Light Heavy leo Jijini Dakar, Senegal.
  Abdelgawwad mwenye umri wa miaka 35 sasa amefuzu kwa mara ya tatu kushiriki Olimpiki kupitia nafasi za 18 za awali kwa Bara la Afrika ambazo zilikuwa zinagombewa na mabondia 235 kutoka mataifa 41 ya Afrika. 
  Baada ya michezo ya kufuzu ya mabara ambayo Afrika ilipewa nafasi chache zaidi katika historia ya Olimpiki, sasa zimebakia nafasi 100 za kufuzu kipitia mashindano ya Kidunia yatakayofanyika Italy mwezi February 2024 na Bangkok, Thailand mwezi April, 2024. 
  Pamoja na hizo kutakuwa na nafasi 9 za upendeleo ambazo pia Changalawe anaweza kubahatika nazo.
  Timu inatarajiwa kuondoka Jiji la Dakar, Senegal alfajiri ya Jumamosi na Shirika la Ndege la Ethiopia kupitia Bamako - Mali na Addis Ababa, Ethiopia kurejea nyumbani, Dar es Salaam.
  Mabondia wengine watano wa Tanzania walitolewa mapema ambao ni Abdallah Katoto na Grace Mwakamele walioishia Robo Fainali, Musa Maregesi na Zulfa Macho Yusufu walioishia 16 Bora na Muharami Mohamed aliyetolewa Raundi ya Pili tu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: CHANGALAWE APOTEZA FAINALI, ASHINDA MEDALI YA FEDHA DAKAR Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top