• HABARI MPYA

  Monday, September 11, 2023

  PAMBA YAANZA NA MOTO LIGI YA CHAMPIONSHIP, YAICHAPA COSMO 4-0


  TIMU ya Pamba Jiji FC ya leo imetumia vyema Uwanja wa nyumbani, Nyamagana Jijini Mwanza kwa ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Cosmopolitan ya Dar es Salaam katika mchezo wake wa kwanza wa Ligi ya NBC Championship.
  Mabao ya Pamba FC leo yamefungwa na Haruna Chanongo, Jamal Mtegeta, Mudathir Abdullah na Lázaro Joseph na sasa timu hiyo inaanzia kileleni mwa Championship baada ya kukamilika kwa mechi za kwanza.
  Matokeo ya mechi nyingine za Ligi hiyo iliyoanza juzi, Mbeya City iliichapa Green Warriors 5-2, Mbeya Kwanza ikatoa sare ya 1-1 na Polisi Tanzania, Copco United ikachapwa 3-2 na Pan Africans juzi.
  Na jana TMA ilitoka suluhu na Stand United, Ken Gold ilitoka 1-1 na Transit Camp, Fountain Gate Talents iliichapa Ruvu Shooting 2-1 na Mbuni FC ikatoa sare ya 1-1 na Biashara United.


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: PAMBA YAANZA NA MOTO LIGI YA CHAMPIONSHIP, YAICHAPA COSMO 4-0 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top