• HABARI MPYA

  Saturday, September 09, 2023

  AZAM FC YAWACHAPA ARTA SOLAR 2-1 WAFUNGAJI FEI NA DUBE CHAMAZI


  TIMU ya Azam FC imeibuka na ushindi wa mabao 2-1dhidi ya AS Arta Solar 7  ya Djibouti katika mchezo wa kirafiki leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam.
  Mabao ya Azam FC yamefungwa na kiungo wa Kimataifa wa Tanzania, Feisal Salum Abdallah dakika ya saba na mhambuliaji wa Kimataifa wa Zimbabwe, Prince Dube Mpumelelo dakika ya 62, huku bao pekee la AS Arta Solar 7 likifungwa na kiungo wa Kimataifa wa Mali, Moussa Coulibaly dakika ya 50.
  Mechi ya leo kwa Azam FC ilikuwa ya kujiandaa na mchezo wao ujao wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania dhidi ya Singida Fountain Gate wiki ijayo, wakati AS Arta Solar 7 inajiandaa na mchezo wa kwanza wa hatua ya mwisho ya mchujo wa kuwania kuingia hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Zamalek ya Misri Jumamosi ijayo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AZAM FC YAWACHAPA ARTA SOLAR 2-1 WAFUNGAJI FEI NA DUBE CHAMAZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top