WENYEJI, Arsenal wametoka nyuma na kuwaadhibu Manchester United kwa kuwachapa mabao 3-1 katika mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa Emirates Jijini London.
Man United ilitangulia na bao la Marcus Rashford dakika ya 27, kabla ya Arsenal kuzinduka kwa mabao ya Martin Ødegaard dakika ya 28, Declan Rice dakika ya sita ya muda wa ziada na Gabriel Jesus dakika ya 11 ya muda wa ziada baada ya kukamilika dakika 90 za kawaida za mchezo.
Kwa ushindi huo, Arsenal wanafikisha pointi 10 na kusogea nafasi ya tano, wakati Manchester United wanabaki na pointi zao sita na kushukia nafasi ya 11 baada ya wote kuchezea mechi nne.
0 comments:
Post a Comment