• HABARI MPYA

  Saturday, September 16, 2023

  MASHUJAA WAPANDA KILELENI LIGI KUU BAADA YA KUICHAPA IHEFU 2-0 KIGOMA


  WENYEJI, Mashujaa wameibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Ihefu SC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Lake Tanganyika mjini Kigoma.
  Mabao ya Mashujaa iliyopanda Ligi Kuu msimu huu yamefungwa na Omary Kindamba dakika ya 18 na Adam Adam dakika ya 80.
  Kwa ushindi huo, Mashujaa wanafikisha pointi saba katika mchezo wa tatu na kupanda kileleni mwa Ligi Kuu wakizizidi pointi moja moja Yanga, Azam na Simba ambazo zimecheza mechi mbilimbili.
  Kwa upande wao, Ihefu SC baada ya kipigo cha leo ambacho kinakuwa cha pili katika mechi tatu wanabaki na pointi zao tatu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MASHUJAA WAPANDA KILELENI LIGI KUU BAADA YA KUICHAPA IHEFU 2-0 KIGOMA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top