• HABARI MPYA

  Saturday, January 15, 2022

  BIASHARA YALAZIMISHWA SARE 3-3 NA KAGERA MUSOMA


  WENYEJI, Biashara United wamelazimishwa sare ya 3-3 na Kagera Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Karume, Musoma mkoani Mara.
  Mabao ya Biashara yamefungwa na Collins Opare kwa penalti dakika ya 49, Baron Oketchi dakika ya 81 na Ambrose Awio dakika ya 83, wakati ya Kagera yamefungwa na Meshack Mwamita dakika ya kwanza, Erick Mwijage dakika ya 33 na David Luhende dakika ya 90 na ushei.
  Kwa matokeo hayo, timu zote zinafikisha pointi 10, Kagera inaendelea kushika mkia mechi 11 na Biashara juu yake nafasi yake ya 15 mechi 12 sasa.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: BIASHARA YALAZIMISHWA SARE 3-3 NA KAGERA MUSOMA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top