• HABARI MPYA

  Sunday, September 24, 2023

  LIVERPOOL YAICHAPA WEST HAM UNITED 3-1 NA KUKAA NYUMA YA MAN CITY


  WENYEJI, Liverpool wameibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya West Ham United katika mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa Anfield.
  Mabao ya Liverpool yamefungwa na Mohamed Salah dakika ya 16, Darwin Nunez dakika ya 60 na Diogo Jota dakika ya 85, wakati bao pekee la West Ham limefungwa na Jarrod Bowen dakika ya 42.
  Kwa ushindi huo, Liverpool inafikisha pointi 16 na kusogea nafasi ya pili, ikizidiwa pointi mbili na mabingwa watetezi, Manchester City baada ya wote kucheza mechi sita, wakati West Han United inabaki na pointi zake 10 za mechi sita pia nafasi ya saba.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: LIVERPOOL YAICHAPA WEST HAM UNITED 3-1 NA KUKAA NYUMA YA MAN CITY Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top