• HABARI MPYA

  Saturday, September 09, 2023

  TAIFA STARS YAWASILI DAR NA TIKETI YA IVORY COAST 2024


  KIKOSI cha timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars kimewasili Alfajiri ya leo Jijini Dar es Salaam kikitokea Algeria ambako juzi kilikata tiketi ya kucheza Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) mwakani, 2024 baada ya sare ya bila kufungana na wenyeji, Algeria katika mchezo wa mwisho wa Kundi F Uwanja wa Mei 19, 1956 mjini Annaba.
  Kwa matokeo hayo Taifa Stars inamaliza na pointi nane, nyuma ya vinara, Algeria wenye pointi 16 na wote wanafuzu AFCON ya Ivory Coast 2023 wakizipiku Uganda iliyomaliza na pointi saba na Níger pointi mbili.
  Mechi nyingine ya mwisho ya Kundi F juzi Níger walichapwa mabao 2-0 na Uganda Uwanja wa Marrakech nchini Morocco.
  Hii inakuwa mara ya tatu kihistoria kwa Tanzania kufuzu AFCON baada ya mwaka 1980 nchini Nigeria na 2019 nchini Misri.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: TAIFA STARS YAWASILI DAR NA TIKETI YA IVORY COAST 2024 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top