• HABARI MPYA

  Wednesday, September 20, 2023

  BARCELONA YAITANDIKA ROYAL ANTWERP 5-0 HISPANIA


  WENYEJI, FC Barcelona wameibuka na ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya Royal Antwerp ya Ubelgiji katika mchezo wa kwanza wa Kundi H Uwanja wa Olímpic Lluís Companys Jijini Barcelona nchini Hispania.
  Mabao ya Barcelona yamefungwa na João Félix dakika ya 11 na 66, Robert Lewandowski dakika ya 19, Jelle Bataille aliyejifunga dakika ya 22 na Gavi dakika ya 54.
  Mechi nyingine ya Kundi H jana, FC Porto ya Ureno iliwachapa wenyeji, FC Shakhtar Donetsk ya Ukraine mabao 3-1 Uwanja wa Volksparkstadion Jijini Hamburg, Ujerumani.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: BARCELONA YAITANDIKA ROYAL ANTWERP 5-0 HISPANIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top