• HABARI MPYA

  Thursday, September 21, 2023

  AZAM FC YAICHAPA SINGIDA FOUNTAIN GATE 2-1 CHAMAZI


  TIMU ya Azam FC imeibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Singida Fountain Gate katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam.
  Mabao ya Azam FC yamefungwa na beki Msenegal, Cheikh Sidibé dakika ya 10 na kiungo mzawa, Iddi Suleiman ‘Nado’ dakika ya 90 ushei, wakati la Singida Fountain Gate limefungwa na kiungo Mtogo, Marouf Tchakei dakika ya Marouf Tchakei dakika ya 57.
  Kwa ushindi huo, Azam FC inafikisha pointi tisa sawa na Yanga na Simba, inabaki nafasi ya tatu ikizidiwa wastani wa mabao, wakati Singida Fountain Gate inabaki na pointi mbili baada ya wote kucheza mechi tatu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AZAM FC YAICHAPA SINGIDA FOUNTAIN GATE 2-1 CHAMAZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top