• HABARI MPYA

  Wednesday, September 06, 2023

  TAIFA STARS YAWASILI SALAMA ANNABA KUIVAA ALGERIA


  KIKOSI cha Taifa Stars kimewasili salama mjini Annaba nchini Algeria kikitokea Tunisia kilipoweka kambi ya wiki moja kujandaa na mchezo wake wa mwisho wa Kundi F kufuzu AFCON 2023 dhidi ya wenyeji kesho Saa 4:00 usiku Uwanja wa Mei 19, 1956.
  Stars iliyo chini ya Kocha Mualgeria, Adel Amrouche inahitaji japo sare kufuzu AFCON ya mwakani nchini Ivory Coast, ambayo itakuwa ni ya tatu Kihistoria baada ya mwaka 1980 nchini Nigeria na mwaka 2019 nchini Misri.
  Kwa sasa Algeria ambayo imekwishafuzu inaongoza Kundi F kwa pointi 15, ikifuatiwa a Tanzania yenye pointi saba, wakati ina pointinne mbele ya Níger wanaoshika mkia kwapointi zao mbili – wakati Uganda itamaliza na Níger siku hiyo hiyo, Septemba 7 Uwanja wa Marrakech nchini Morocco.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: TAIFA STARS YAWASILI SALAMA ANNABA KUIVAA ALGERIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top