• HABARI MPYA

    Sunday, September 17, 2023

    COASTAL UNION YASAINI MKATABA YA UDHAMINI NA MAKAMPUNI MAWILI


    KATIBU Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Saidi Yakubu ametoa wito kwa makampuni mbalimbali ndani na nje ya Tanzania kujitokeza kudhadhili vilabu vya soka na michezo mbalimbali nchini ili ziwe na ushindani  katika medani za kitaifa na kimataifa.
    Katibu Mkuu, Yakubu ametoa wito huo jijini Tanga akiwa Mgeni Rasmi wakati timu ya Coastal Union ilipokuwa ikisaini mkataba na kampuni ya Elsewedy Electric Cable East Africa Ltd ambayo itaifadhili timu hiyo kwa msimu wa 2023/2024 pamoja na kuzindua jezi itakayotumika kwa msimu huu.
    "Mpira sasa unahitaji vitu vitatu, ufundi kwa maana ya utaalam wa michezo kwa wachezaji na viongozi, vipaji vya wachezaji vinavyokuzwa na kulelewa na kuwaandaa kuwa wachezaji bora ambao watumiwa na vilabu, timu ya taifa na hata soka la kulipwa nje ya nchi pamoja na fedha ambazo ndiyo chachu ya soka na michezo mingine kwa kuzingatia michezo ni ajira" amesema Katibu Mkuu, Yakubu.
    Amewataka uongozi wa timu ya Coastal Union kutumia fedha zitakazotolewa na wafadhili hao kwa malengo yaliyokusudiwa kwa kuweka mikakati mizuri ya ushindi.
    Aidha, ametoa wito kwa Mfadhili huyo Mpya na kusisitiza kuwa Coastal Union ni dude lililolala, ufadhili wao na utaalam utaiamsha timu hiyo ili ifanye vizuri katika medani ya soka kwa kuzingatia Misri ni taifa kubwa kisoka barani Afrika na kuwataka waisaidie timu hiyo kupate wasaa wa kuwa na maandalizi mazuri ya msimu ujao kwa kuwapa nafasi ya kuweka kambi nchini Misri.
    Kwa upande wao Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Elsewedy Electric East Africa Mhandisi Ibrahim Qamar na Mkurugenzi wa Biashara katika Miradi, Muhammad El Shazly wamesema wanafuraha kufanya kazi na timu ya Coastal Union kwa kuwa historia zao zinafanana,  kampuni hiyo imeanzishwa mwaka 1938 na timu ya Coastal Union imeanzishwa 1948.
    Kwa upande wake Mwenyekiti wa timu hiyo Steven Mguto amesema ufadhili ambao wamepata utasidia timu hiyo kutekeleza majukumu yake ya msingi ambayo ni kuijenga timu iwe na ushindani na kushika nafasi nne za juu katika ligi ya NBC ili mwakani washiriki mashindano ya kimataifa.
    Katika hatua nyingine, Coastal Unión imesaini mkataba na kampuni ya  K4 Security ambao utafanya kambi klabu hiyo na misafara yake yote ya kuwa chini ya ulinzi wa kampuni hiyo.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: COASTAL UNION YASAINI MKATABA YA UDHAMINI NA MAKAMPUNI MAWILI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top