• HABARI MPYA

  Saturday, September 02, 2023

  NI SIMBA SC NA AL AHLY YA MISRI LIGI YA CAF OKTOBA


  KLABU ya Simba itaanza na mabingwa wa Afrika, Al Ahly ya Misri katika michuano mipya ya Ligi ya Soka Afrika ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF), maarufu kama CAF African Football League inayotarajiwa kuanza mwezi ujao.
  Wekundu hao wa Msimbazi wataanzia nyumbani Oktoba 20 Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam katika mchezo rasmi wa ufunguzi inayoanzia hatua ya Robo Fainali kwa njia ya mtoano hadi Fainali.
  Mechi ya marudiano itafuatia Jijini Cairo na wakifuzu Nusu Fainali itachezwa Oktoba 29 na Novemba 1, wakati Fainali ni Novemba 5.
  Mechi nyingine za Robo Fainali TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo itaanzia nyumbani dhidi ya Esperance ya Tunisia, Enyimba ya Nigeria itaanzia nyumbani dhidi ya Wydad Athletic ya Morocco na Petro Atletico ya Angola itaanzia nyumbani dhidi ya Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: NI SIMBA SC NA AL AHLY YA MISRI LIGI YA CAF OKTOBA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top