• HABARI MPYA

  Wednesday, September 13, 2023

  LIGI YA NBC CHAMPIONSHIP KUONYESHWA KWA SH MILIONI 613 MIAKA MITATU


  SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limeingia mkataba wa miaka mitatu na Kampuni ya Startimes kuonyesha Ligi ya NBC Championship (NBCCL) wenye thamani ya Shilingi Milioni 613 kuanzia msimu huu.
  Makubaliano hayo ya thamani ya shilingi za Milioni 613 za Kitanzania na Kampuni ya Startimes ni kuonyesha mubashara mechi 170  za Ligi ya NBC Championship kuanzia msimu wa 2023-2024 kwa kupitia chaneli ya TV3.
  Akizungumza na wanahabari Leo  Septemba 13,2023 Rais wa Shirikisho la mpira wa miguu nchini Wallace  Karia amesema ndani ya miaka 11 Leo imekuwa mara ya pili kuingia makubaliano ya kuruhusu wadau kurusha matangazo ya mpira wa miguu (NBC CHAMPIONSHIP).
  “Tutakuwa pamoja katika uongozi wangu sisi ni waungwana nathamini Tv3 kuja wakati Championship ikiwa katika kipindi kigumu hivyo mtaendelea kuwa kipaumbele chetu kwa miaka ijayo baadae mambo yakiwaka najua watu watakuja lakini sisi tutawapa kipaumbele Tv3. 
  “Tv3 itafika mbali na Championship itafika mbali pia Mkataba huu ni wa miaka 3 wenye thamani ya milioni 613 za kitanzania, amesema Wallace Karia Rais wa TFF."
  Karia ameeleza kuwa Ligi hiyo ni miongoni mwa ligi ya 5 kwa ubora Afrika hivyo inaenda kuwapa fursa watu wengi Duniani kushuhudia vitu mbalimbali na ugumu wa ligi hiyo huku akiwatia moyo wadhamini hao (TV3) Kuwa kwa sasa Kuna miundombinu mizuri kwenye viwanja vilivyokidhi vigezo tayari kwa mechi hizo za Nbc championship.
  Nae Meneja Masoko wa Kampuni ya Startimes David Malisa ameeleza namna Tv3 ndani ya Kisimbuzi cha Startimes inakuwa kwa kasi na ndio tv3 yenye miaka miwili tangu kuanzishwa kwake lakini tayari imeonesha michuano mbalimbali ndani na nje ya nchi.
  Aidha,Malisa ameongeza kuwa watatoa ushirikiano wa Hali ya juu na mashabiki wa soka wategemee kuona picha angavu zenye ubora zaidi kama ilivyo dhamira ya Kampuni hiyo kuhakikisha mlaji anapata kilichobora siku zote.
  Pia ameeleza kuwa mbali na mashabiki kupata fursa ya kushuhudia mubashara michuano hiyo pia watapata nafasi kila mkoa kutoa maoni ya namna ya mienendo ya ligi hiyo inavyokwenda na nini kifanyike ili kuwepo na maboresho mbalimbali. 
  Kwa Upande wake Msimamizi wa vipindi kutoka Tv3 Emmanuel Sikawa amesema ni hatua kubwa kufikia makubaliano hayo yenye tija na lengo la kukuza na kuinua mchezo wa soka la Tanzania. 
  "Tumejipanga kutoa madhui ya Ligi hiyo ya Nbc Championship 2023 kwa mechi zisizopungua 170 mubashara na tutegemee vilabu mbalimbali vinaenda kunufaika kupitia makubaliano haya".
  Hata hivyo Sikawa amewataka mashabiki wa michezo nchini kukaa tayari kwani wamejipanga vizuri kutoa maudhui ya kimichezo na hivi karibuni itawajia Tv3 Sport lengo ni kuweka Maudhui yote ya kimichezo kwa undani zaidi.
  Aidha katika kuhakikisha ligi inakuwa bora tv3 na StarTimes tumejipanga kwelikweli na chaneli zote mbili za Tv3 na Tv 3 Sports zitakuwa kwenye mfumo wa picha angavu,” amesema Malisa.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: LIGI YA NBC CHAMPIONSHIP KUONYESHWA KWA SH MILIONI 613 MIAKA MITATU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top