• HABARI MPYA

  Saturday, September 30, 2023

  WAWILI KADI NYEKUNDU LIVERPOOL YACHAPWA 2-1 TOTTENHAM


  WENYEJI, Tottenham Hotspur wameibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Liverpool katika mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa Tottenham Hotspur Jijini London.
  Mabao ya Tottenham Hotspur yamefungwa na Son Heung-Min dakika ya 36 na Joel Matip aliyejifunga dakika ya 90 na ushei, wakati bao pekee la Liverpool limefungwa na Cody Gakpo dakika ya 45 na ushei.
  Liverpool ilimaliza mchezo huo pungufu baada ya wachezaji wake wawili kutolewa kwa kadi nyekundu, Curtis Jones dakika ya 26 na Diogo Jota dakika ya 69.
  Kwa ushindi huo, Tottenham Hotspur inafikisha pointi 17 na kusogea nafasi ya tatu, wakati Liverpool inayobaki na pointi zake 16 inashukia nafasi ya nne.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: WAWILI KADI NYEKUNDU LIVERPOOL YACHAPWA 2-1 TOTTENHAM Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top