• HABARI MPYA

  Saturday, September 09, 2023

  KONKONI NA MUSONDA KILA MMOJA APIGA MBILI YANGA YASHINDA 6-0


  MABINGWA wa Tanzania, Yanga SC wameibuka na ushindi wa mabao 6-0 dhidi ya Kiluvya United katika mchezo wa kirafiki leo Uwanja wa Avic Town, Kigamboni Jijini Dar es Salaam.
  Mabao ya Yanga yamefungwa na viungo wazawa Farid Mussa na Crispín Ngushi moja kila mmoja na washambuliaji Mghana, Hafiz Konkoni na Mzambia, Kennedy Musonda kila mmoja mawili.
  Yanga SC inajiandaa na mchezo wake wa kwanza wa Raundi ya mwisho ya mchujo wa kuwania kuingia hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya El Merreikh ya Sudan Septemba 16, mwaka huu Uwanja wa Pele Jijini Kigali nchini Rwanda.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KONKONI NA MUSONDA KILA MMOJA APIGA MBILI YANGA YASHINDA 6-0 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top